
Mapenzi ni kama kikohozi na kweli wawili wakikosana nenda ukalime, wakipatana nenda ukavune.
Msanii Otile Brown amerudiana na mpenzi wake wa Uhabeshi Nabayet aliyeachana naye miezi michache zilizopita.
Nabayet alimwacha Otile Brown kwa madai ya uaminifu kwenye uhusiano wao na kusema kuwa mapenzi sio ya kuyachezea.
“Moyo wangu kamwe utakudundia lakini kwa sasa maisha yametuleta hapa. Nashukuru kwa kujaribu, kwa kweli nashukuru. Inachukua kiasi kikubwa kwa mwanaume kuchukua muda na kuomba msamaha. Labda siku moja tutapatana kwa tena. OB ninakushukuru sana, kamwe nitakuombea na kukutakia mazuri kwenye maisha,” Nabayet alimwandikia Otile Brown baada ya kutungiwa nyimbo ya msamaha.
Juhudi za Otile Brown kumrudia mpenzi wake ziligonga mwamba bazda ya kumtungia wimbo wa kumwomba msamaha.
Lakini kama kitu ni chako huwa ni chako, Otile Brown hatimaye amefanikiwa kumrudia Nabayet na wote wameanza kutisha kwenye mitandao ya kijamii.
“Mapenzi ya kweli hayana udhaifu! Mwaka moja umeisha na natazamia miaka na mikaka mpenzi wangu,” Nabayet aliyaandika maneno haya kwenye Instagram.
Tazama video hii ya Otile Brown na Nabayet wakipiga densi;