Msanii maarufu wa injili anayeishi nchini Nigeria, Emmy Kosgei alisherehekea kumbukumbu ya ndoa yake.
Emmy Kosgei aliolewa na mhubiri wa Nigeria, Anselm Madubuko, mnamo 2013 katika harusi ya hali ya juu.
Siku ya Jumamosi, Emmy na mume ake waliadhimisha mwaka mwingine wa umoja wao na upendo.
Kheri ya siku ya maadhimisho kwetu. Mungu amekuwa mwaninifu ! Amadubuko nakupenda kila wakati… Nina furaha sana maana niliitikia wito wako.
Emmy na mumeo hawana watoto hadi sasa na katika mahojiano yaliyopita mwaka jana, mwanamuziki wa Kalenjin alisema kwamba hana haraka kuzaa watoto.
Sikuolewa kwa sababu tu nilitaka kuwa ns watoto. Mahusiano ni juu ya umoja na kupendana milele. Ikiwa umeunganishwa na mtu mbaya, inaweza kuathiri hatima yako milele
Emmy anawalea watoto wake wa kambo ambao anasema “wananiita mama na ninawapenda”
Leave a Reply